Wednesday, May 22, 2013

BRAND NEW SONG: ABBY SKILLS FEAT CHEGGE / SHANNY NA JENNY


PICHA NA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA VURUGU ZA MTWARA

 
Taarifa zinaripoti kwamba hali sio nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo. Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam. Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam. Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi) Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto. Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika. Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi) Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupitakwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi. Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi) Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao. Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia. Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate. Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa. Wakati waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni" Wananchi walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. Hatimaye hivi Punde matangazo yarejea. Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni. Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara. 

 

SOURCE:Dartimes.com

Tuesday, May 21, 2013

NEW JOINT: ATTENTION / MRAP FEAT DEDDY

                          


      From B hitz Produced By Pancho Latino

UTATA WA TOUR YA JAY Z TO TZ

Bado wataalam wa mambo wanaendelea kutofautiana kuhusu ratiba ya Tour ya Jay – z iliyotolewa na Billboard hivi karibuni katika ratiba hiyo imeandikwa Jay z atatua katika miji 7 ya Africa ikiwemo jiji la Dar es salaam Oktoba 4 mwaka huu pale Diamond Jubilee. Ratiba hiyo inatia shaka kwa sababu Jay z aliperform tarehe na mwezi kama huo Dar es salaam mwaka 2006 na katika website ya Jay za ametoa ratiba ya Tour zake laini ameishia kuandika mwezi Septemba hajaandika mpaka Oktoba kama walivyoandika Billboard.
SOURCE:Dj Fetty

NEW VIDEO:TZ ALL FEMALE STARS-KIDOLE KIMOJA (FISTULA OFFICIAL VIDEO)

 


Tz All Female Stars
Kidole Kimoja.(FESTULA)
Studio:Surround Sound Studio
Prod:Nash Designer
Dir:Sadiki Hamadi & Peter Mbogo
Redline Production

SABABU ZA MSANII PROFESA JAY KUCHUKUA KADI YA CHADEMA....HIKI NDO ALICHOKISEMA

 Mh Sugu,Profesa Jay na Mh John Mnyika leo Dodoma.
Profesa Jay amesema yeye ni mwanaharakati muda mrefu na amejiunga na amejiunga na CHADEMA rasmi leo lakini yeye ni mfuasi wa Chama hicho muda mrefu kutokana na harakati zake za kutaka kuikomboa Tanzania.Profesa Jay alisema kuwa anapenda Tanzania Bora,na anaamini Chama cha Chadema kina muelekeo huo wa kuipeleka Tanzania kuwa Bora.Hiyo ndo maana ameamua kuchukua kadi ya chama hicho na si kwa nia ya kufanya Siasa ila ni kwaajili ya kuijenga Tanzania na kuendeleza harakati.

Sunday, May 19, 2013

PHOTO:Wiz Khalifa n' Amber Rose @ the 2013 Billboard Awards

 
(photo courtesy of Just Jared).,

PHOTOS:Kanye West New Album Art is…Interesting

kanye-west-debuts-black-skinhead-on-saturday-night-live-finale-1 


(AllHipHop News) Kanye West is on a roll.  He debuted two new songs and announced the release date of his new album (June 18th). Hours after his performance on the season finale of Saturday Night Live Mr. West is now giving us the name of his latest LP – Yeezus.
KanyeWestalbum