Wednesday, July 24, 2013

NEW VIDEO:Beeman feat wyre - Kizunguzungu|Good Music|All the Way From Arusha


Beeman feat wyre - Kizunguzungu

Cpwaa Breaks|Sasa nyimbo zake zaanza patikana on "iTunes"....Check out hapa


Cpwaa Universal Music 2
Cpwaa anakwambia…. Ninayo furaha kuwajulisha kwamba sasa kazi zangu zote za muziki zitakuwa zinapatikana kwenye mitandao yote ya kununua nyimbo za wasanii duniani. Tayari nishasambaza Album yangu ya kwanza ” Pwaa The Album” na singles zingine kama “Hmmm”, na “Mambo” kwenye mitandao ifuatayo:
iTunes, Amazon MP3, Spotify, Google Play, Xbox Music, Deezer, Rhapsody, Simfy, MySpace Music, Nokia, Wimp, Sony Music Unlimited,Napster, Verve Life, Media net, Shazam,eMusic, iHeartRadio, Muve Music, and Rdio.
kwa wale mliokosa nafasi ya kujipatia nakala za album yangu ya kwanza, hii ni fursa kwenu kujipatia Album hiyo kupitia mitandao hii kwa bei nafuu sana. Tupeane support ili tukuze muziki wetu.
kwa sasa namalizia kurekodi album yangu ya pili ambayo ipo kwenye mahadhi ya kimataifa zaidi na punde ikikamilika ntaanza kuachia single moja moja kupitia mitandao hii, mitandao ya simu kwa njia ya RBT na pamoja na wa “The Kleek” chini ya mkataba wangu mpya na Universal Music Group.
Asanteni sana na hii hapa ni link ya kupata nyimbo zangu zote kupitia iTunes, https://itunes.apple.com/album/pwaa-the-album/id676185780
cp music

Inspired By Technology:Sasa waweza kupima Malaria kwa kutumia Hii Application|Soma Zaidi Hapa.


mini-IMAGINE2-e1374124657569
Sanyansi na teknolojia ndio vitu vinavyo run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana na ugunduzi ambao Microsoft wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola za Kimarekani elfu kumi na mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo, hivi sasa inawezekana kupima malaria bila hata kutoa damu lakini hapohapo doctor wako akatumiwa taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya  Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu kwa sasa inafanya kazi  na windows phone lakini ili uweze kupima malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.
safe_image 
Credits:Millard Ayo

#SIMCARDTAX:RAIS KIKWETE|SOMA ALICHOKISEMA

B
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam  Julai 23, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.



Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.



Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.



Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.



“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,”Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.



Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.



23 Julai, 2013

PICHA NA VIDEO:PRINCE William& Kate Middleton wakimuonyesha mtoto wao Hadharani.

p-9Hapa Kate Middleton na mtoto wake aliyepewa Jina la George Alexander Louis Siku Mbili baada ya kuzaliwa kwakep-5Prince William akiwa na familia yake saa24 baada ya mtot wao kuzaliwap-4Hali ilivyokuwa njee ya hospitali St.Marry's Hospitalp-24hapa wakiondoka Hospitalini Hapop-25        Video ya tukio zima angalia hapa chini

Ney Lee - Nipe Muda

Ney Lee 


Staa wa Ngoma ya Umekweenda alichipukia kutoka kwenye Fiesta Super Nyota na kufanya vizuri sasa aachia another Hit Song NIPE MUDA Isikilize hapo chini.

FiDO & Danger Ranger - Tupo Tulipo (Official Music Video) Another HipHop MUsic From Arusha.


Artist:FiDO & Danger Ranger

Song:Tupo Tulipo

Audio:MAJEMBE RECORDS.

Video:Good Pictures Lab (First Music Video Project)

Please leave up your comments.

PICHA:UKIONA HII DRESS CODE UJUE INAWAKILSHA ARUSHA|Unga Ltd

 


     Hapo Kuanzia Juu ni Boshori,DoggyDoggy+Denim Shirts na Chini Trouser Mnyonyo na                Converse All Star Oversive Wanasemaga haina Gweraaaa

MUSIC VIDEO:KELLY ROWLAND - Dirty Laundry

MUSIC VIDEO:ZaiiD - WHO DAT(Bongo version) Shot in Iringa Ni nzuri good idea.

zaiid
ZaiiD - WHO DAT(Bongo version)