Showing posts with label mlipuko olasiti. Show all posts
Showing posts with label mlipuko olasiti. Show all posts

Monday, May 13, 2013

MTUHUMIWA NAMBA MOJA WA BOMU LA ARUSHA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO NA KUSOMEWA MASHITAKA 21

 
 Mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya mauaji na kujaribu kuua.

Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.

Mawakili wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo makosa mengine bado hayajatajwa..




Pia polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol), kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa hilo.

Thursday, May 9, 2013

ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO | YASOME HAPA

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.



Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.

Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo,  walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.