Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Wednesday, August 7, 2013

VIDEO:TUKIO ZIMA LA MOTO UWANJA WA NDEGE JOMO KENYATTA LEO ASUBUHI.


Hii ni video ya tukio zima la mlipuko wa moto uliotokea leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta

Wednesday, July 24, 2013

#SIMCARDTAX:RAIS KIKWETE|SOMA ALICHOKISEMA

B
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam  Julai 23, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.



Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.



Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.



Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.



“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,”Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.



Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.



23 Julai, 2013

Friday, July 19, 2013

NAMBA ZA SIMU ZA MAWAZIRI ILI KUWATUMIA MAONI KUHUSU KODI YA SIMU


Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644. Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa. 



Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013

FAHAMU:CHADEMA YAJITOA KUWANIA UMEYA WA ARUSHA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeamua kuachana na kuwania umeya wa Jiji na badala yake kimemwomba Meya, Gaudence Lyimo (CCM), atende haki.

Katibu wa Kanda ya Kaskazini wa chama hicho, Amani  Golugwa alisema jana, kwamba Chadema haina uroho wa madaraka kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali inasimamia vipaumbele vya maendeleo.


Hata hivyo, kauli hiyo inapingana na nyingine ya chama hicho ya wiki hii pia, kwamba ushindi katika uchaguzi mdogo wa kata nne, ni chachu katika msimamo wa chama kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, urudiwe.

Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema, Isaya Doita, ndiye aliyenukuliwa wiki hii akisema hayo, akiamini kuwa Meya Lyimo wa CCM, alichaguliwa kimizengwe.

Baada ya Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa hivi karibuni, kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha, huku CCM ikibaki na viti 12 na TLP sita.
 

Pia Chadema ina nafasi ya kuongeza kiti, kwani ina nafasi moja ya viti maalumu iliyokuwa inakaliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka 2011.

Hata hivyo, pamoja na Chadema kuongoza kwa kuwa na viti vingi vya udiwani jijini hapa, haina uwezo wa kuweka Meya, bila kushirikiana na CCM au TLP.

Chadema ikikosa ushirikiano huo, ushirikiano wa CCM na TLP, utabaki kuwa na nguvu ya kuweka Meya na naibu wake madarakani, huku Chadema ikibaki kuwa kambi ya upinzani yenye nguvu katika Baraza la Madiwani.

Golugwa alisema Chadema haina uroho wa madaraka, bali inataka uchaguzi wa Meya wa Jiji urudiwe ingawa haitaki nafasi hiyo kwa kuwa si kipaumbele chake.
 

"Tunaangalia wananchi wanafikiwaje na maendeleo tuna imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria," alisema Golugwa.  
 

"Hatuna shida na Meya wala hatuna uroho wa madaraka tunachopinga ni upatikanaji wa Meya huyo na tunamtaka afanye kazi zake kwa kusimamia misingi ya sheria na si upendeleo, tunahitaji kuona kila mwananchi ananufaika na maendeleo hadi mitaani," aliongeza.

Pia alikaririwa wakati mmoja akisema ushindi huo unaihakikishia Chadema wingi wa wajumbe katika Baraza  la Madiwani, hivyo kuwa na fursa ya kumwondoa Lyimo madarakani.

Thursday, July 18, 2013

RAIS KIKWETE AMTAKA RAIS WA SUDAN AWASAKE WATU WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA HARAKA IWEZEKANAVYO


Rais Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan, Omar Bashir, kuhusu kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur.

Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Rais  Kikwete alimtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu, na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

Rais Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alimueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini waliohusika ni wahalifu, kusisitiza kuwa lazima watasakwa hadi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Alimpa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha, ambapo wanajeshi wa Tanzania walienda nchini Sudan kulinda amani na usalama wa wananchi wa Sudan.

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha, ambao umewatokea Watanzania hao wakati wakitekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichokiri kuhusika na shambulio hilo, ingawa kumekuwa na hali ya kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na vya waasi katika jimbo la Darfur.

Mapigano baina ya vikundi vya kikabila na koo mbalimbali, yamesababisha mapigano na uvunjifu mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa.

Mara nyingi mapigano na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.

Mwishoni mwa mwaka jana wanajeshi wanne kutoka Nigeria, waliuawa karibu na El Geneina, Magharibi mwa Darfur, ambapo pia inaelezwa na AU kuwa wanajeshi wapatao 50, wameuawa tangu kikosi hicho cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID), kianze operesheni yake mwishoni mwa 2007.
 

Taarifa za UN pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania Jumamosi iliyopita, wanajeshi sita wanaolinda amani waliuawa tangu Oktoba mwaka huu, ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao.
Hata hivyo, kiini cha mgogoro huo inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

Miili ya maaskari hao saba wa Tanzania, inatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa, Julai 19 kwa ajili ya maziko.
Credit:Gumzo La Jiji

HAPPY 95th BIRTHDAY NELSON MANDELA (MADIBA)

 




Afrika Kusini leo wanasherehekea miaka 95 ya kuzaliwa kwa Mzee Nelson Mandela huku rais huyo wa zamani bado yuko mahututi hospitalini.
Ilikuwa ikitabiriwa kwamba shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwamba angeruhusiwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini bado yuko hospitali kutokana na kurejea maambukizi kwenye mapafu.


Kituo cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela na makundi mengine yamewataka watu kujitolea kwa dakika 67 kwa kazi za hisani kukumbukia miaka 67 ambayo Mandela aliitumikia jamii yake.

Umoja wa Mataifa pia umetambua mapambano ya Mandela dhidi ya ubaguzi wa rangi na kusema siku yake ya kuzaliwa ni fursa ya kuenzi urithi wake, na shughuli mbalimbali zimeandaliwa duniani kote.

Siku ya kuzaliwa Mandela, Julai 18, ilitangazwa rasmi kuwa Siku ya Kimataifa ya Mandela na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2009 kama kutambua mchango wake kwa utamaduni wa amani na uhuru.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alisema Siku ya kuzaliwa Mandela mwaka huu imekuja katika wakati wa 'kuakisi kwa kina maisha yake na kazi ya Madiba, huku kiongozi huyo wa aina yake akiwa bado yuko hospitalini'
Aliongeza: "Nelson Mandela alijitolea miaka 67 ya maisha yake kupigania haki za binadamu na haki kwa wote."


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ataadhimisha siku ya kuzaliwa Mandela kwa kutoa michango ya nyumba kwa familia masikini katika eneo la Pretoria.

Mandela alilazwa hospitali mjini Pretoria Juni 8 kwa matatizo ya maambukizi kwenye mapafu yake.

Mapema wiki hii, Rais mstaafu Thabo Mbeki alibashiri kwamba Mandela anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali mapema na kwenda kupatia nafuu nyumbani.

Marafiki ambao walimtembelea wamesema yuko kwenye mashine ya kusaidia maisha kwa ajili ya kusaidia tu kupumua kwa urahisi.
 

Taarifa rasmi za hivi karibuni kabisa kuhusiana na afya yake zilisema Mandela alikuwa kwenye hali mbaya lakini inayoimarika.

Lakini wote, mke wa Mandela, Graca Machel, na Rais Jacob Zuma wamesema hivi karibuni kwamba Mandela anaendelea vema na matibabu.

Shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi alitumikia miaka 27 gerezani kabla ya kuja kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994

Monday, July 15, 2013

PICHA:WANAJESHI 7 WA TZ WALIOFARIKI DARFUR WAKIAGWA HUKO TAYARI KWA KUSAFIRISHWA

Hundreds of UNAMID Sector South HQ staff members led by Head of Office Mr. Imtiaz Hussain today attended a brief ceremony at the Pakistan Level III Hospital in Nyala to pay their final respects to the seven Tanzanian peacekeepers who were killed near Khor Abeche in an ambush by unidentified gunmen on Saturday 13 July 2013.Their bodies were flown today to Khartoum en route to Tanzania.
Top Sector leadership led by Mr. Hussain (3rd R)
UNAMID JSR Dr. Mohamed Ibn Chambas along with Acting Force Commander Lt. Gen. Wynjones Kisamba and Police Commissioner Ms. Hester Adriana Paneras visited the other 17 injured peacekeepers at the same Hospital yesterday.

The Mission leadership and the UNSG Ban Ki-moon have condemned the act and called for the Government of Sudan to bring the perpetrators of the “heinous” act to justice.Meanwhile, according to press reports, Tanzanian President JakayaKikwete expressed his deep shock following the incident and he sent condolences to the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) and the bereaved families.
Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony

He wished quick recovery for the injured soldiers, saying: “I don’t have a lot of words to express my shock and sadness on the soldiers who died while on a very important mission of United Nations, on keeping peace in an area where thousands of people have been killed…” Mr. Kikwete said in a statement issued by the Directorate of Presidential Communications yesterday, adding; “since the fallen servicemen and women were deployed in Darfur in February this year and since Tanzania  started deploying troops in 2007, they have done a good work and the country is proud of them”. 
A portion of  staff members at the ceremony

The TPDF Spokesperson, Lt. Col. KapambalaMgawe, said during a press conference yesterday that a special delegation has been sent to Khartoum and Darfur to talk with the authorities over the incident. Tanzania has a battalion of about 850 peacekeepers in Darfur located at Khor Abeche and Menawashi, South Darfur State.

Military salute as the 'Last Post'  rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers
Prayers from a chaplain
Prayers from another  chaplain
Maj. Elinami Moshi reads brief CVs of the deceased to the top brass
A section of the top brass
Last Post
Start of the last journey home
Credit:Michuzi Blogs & TZ Daily Eye

Sunday, July 14, 2013

FAHAMU: Matokeo ya Uchaguzi katika Kata Nne za Arusha

Uchaguzi uliofanyika leo Jumapili, Julai 14, 2013 wa kuwapata madiwani wa Kata Nne --Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai-- za mkoani Arusha umemalizika.

Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne kama ifuatavyo:

KATA YA THEMI: CHADEMA 678; CCM 326; CUF 313

KATA YA KIMANDOLU: CHADEMA 2,665; CCM 1,169

KATA YA KALOLENI: CHADEMA 1,019; CCM 389; CUF 169

KATA YA ELERAI: CHADEMA 1,715; CCM 1,239; CUF 213

Vyama vingine vilivyoshiriki vilikuwa ni TLP, CCK na Demokrasia Makini

MAJINA SABA YA WANAJESHI WA TANZANIA WALIO UAWA HUKO DARFUR SUDANI


Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa  kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.


Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati  wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
 
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

PICHA:Uchaguzi Mdogo ARUSHA

FAHAMU:SHEIKH MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUMIZWA VIBAYA


Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.

Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.

Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.

Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.

Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu
huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.


‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa  akilia.

Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na  mgongoni, pia ana majeraha  kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.

Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.

Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.

Kwa upande wake,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna  mtu anayeshikiliwa hadi sasa.

FAHAMU:WANAJESHI 7 WA TANZANIA WAMEUAWA HUKO DARFUR - SUDAN


Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.


Taarifa zilizotufikia jana  zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.



Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.



Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.



Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.



Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.



Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.



Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.


Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.


Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.



Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.



Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850.

“Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.

“Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema.

Saturday, July 13, 2013

HUYU NDIYE BABU ANAYETAKA KUMFUFUA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ILI ASIMAMIE UCHAGUZI MKUU 2015, AZUA GUMZO KUBWA..!!


Mzee (pichani) aliyeibuka hivi karibuni akidai kuwa ana uwezo wa kumfufua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere amezua gumzo.
 Babu huyo aliibuka katika studio za Kyera FM huko mkoani Mbeya akihitaji msaada wa kumfikisha Butihama alipozikwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999 ili amfufue. 


Mzee huyo alikuwa na ufunguo mkononi ambao anadai ndiyo utakaotumika kumfufua Nyerere. Anaeleza kuwa akishamfufua Mwalimu Nyerere ndiye atakayesimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Thursday, July 11, 2013

FAHAMU:Kauli Ya POLISI Tanzania kuhusu CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami

.
.
Ni kauli ya Polisi kutoka Makao Makuu Dar es salaam na imetolewa kutokana na kauli iliyokaririwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe..
.
.
. 
Credit:Millad ayo

Friday, July 5, 2013

ALICHOKIANDIKA Mh. Zitto Kabwe kuhusu kodi mpya ya Tshs. 1,000/= kwa mwezi kwa kila laini ya simu

Maneno haya yameandikwa na Mh. Zitto Kabwe, jana tarehe 4 Julai kupitia akaunti yake ya Facebook:
“Kodi ya Tshs 1,000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na Wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili. Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.”
Zitto FB
S

FAHAMU:Rapper WAKAZI KU-PERFOM KWENYE BBA"The Chase" Eviction Party Wikiendi hii

wakazi
Tanzania’s own ‘Bilingual Beast’, Wakazi, will storm the stage during Sunday night’s Big Brother: The Chase eviction show, live on AfricaMagic Entertainment and DStv Channel 197 & 198 from 20:00 CAT. Famed for his fearsome rhymes in Swahili and English, Wakazi will keep the energy high as audiences across the continent wait to see which housemates will be evicted from The Chase this week.
Wakazi has come a long way since he started rapping at high school talent shows. With his focus shifted elsewhere by his family, he never took music seriously – until he relocated to Chicago and his love for Hip Hop was rejuvenated. He’s subsequently released three mixtapes, performed at festivals in North America and opened for megastars like Ice Prince and 2Face Idibia.

His signature blend of English and Swahili rhymes won him the nickname ‘Bilingual Beast’ and his ability to tell a story and mesmerizing manipulation of words and metaphors mark him out as a true creative force.
You won’t want to miss Wakazi’s lyrical Hip Hop stylings this Sunday – and don’t forget to vote to keep your favourite housemate in The Chase! The housemates in danger of eviction are Angelo, Fatima, Bimp, Cleo, Pokello, Hakeem, and Nando. Voting is open now and closes at 06:00 CAT on Sunday morning
Meanwhile, in other Big Brother news, Tumi Morake host of Big Brother Hot Room will also be making a guest appearance on StarGist, Friday 5 July at 19:30 CAT on AfricaMagic Entertainment. The South African comedienne will be talking about her life and career as well as giving an insight into the work that goes into putting the weekly satirical show together.
Big Brother: The Chase is headline sponsored by Airtel and produced by Endemol South Africa

Wednesday, July 3, 2013

Ray C Instagram Check alichokisema.

Mwanadada Ray C leo hii kupitia ukurasa wake wa instagram ameachia ujumbe huu kwaajili ya mashabiki zake na kuwashukuru kwa support yao. Ametirikia hivi:

FAHAMU:Cpwaa Asaini na Universal Music Group...Soma na Sikiliza alichokisema HAPA.

.
CPwaa Interview Channel O – Africa Music Video Awards 2012
The Tanzanian International Bongoflava Artist has signed a licensing deal with one of the world biggest and top Music labels “Universal Music, South Africa”. His content will be distributed through the Kleek, a mobile streaming service available on all Samsung smart phone in Ghana, Angola, Kenya, South Africa and Nigeria. CPwaa is one of the A-List Artists signed by Universal Music from East Africa for its Kleek continental platform.
On March 13, 2013 Universal Music Group, in partnership with Samsung, as well as African and international music labels and publishers, has launched a pan-African mobile music streaming service called the Kleek. Designed and built specifically for Africa, the Kleek will bring music lovers closer to their favorite artists, while also providing artists with valuable access to a wider pan-African audience.
 cpwaa3
This new deal will make CPwaa not only to gain more revenues from his music but also a worldwide exposure and global outreach through the Kleek.
To learn more about the Kleek go here
http://thekleek.com/
http://www.universalmusic.com/corporate/detail/2458
http://www.theverge.com/2013/3/14/4103286/universal-music-samsung-the-kleek-music-streaming-africa
Source:Millard Ayo

Tuesday, July 2, 2013

PICHA ZA GEORGE BUSH ALIPOKUTANA NA RAIS OBAMA TANZANIA KABLA HAJAONDOKA

 Rais Obama pamoja na Bush walikutana leo Asubuhi katika Ubalozi wa Marekani uliopo jijini Dar es Salaam na kufanya tendo la kutoa heshima zao kwa Walipoteza Maisha pamoja na wale wote walioathirika katika shambulio la Ugaidi katika Ubalozi wao hapa nchini mwaka 1998.



DIAMOND AANIKA JUMLA YA MAPATO YAKE ALIYOINGIZA KWENYE SHOW ZA MWEZI ULIOPITA WA JUNE..!!

Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi.


Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.
Show ya nchini Comoro 22 June
Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38.
Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June
Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15.


Show ya Tigo Mwanza 30 June
Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10.
Kili Music Tour 2013
Tulipata taarifa kuwa Diamond atafanya show kwenye mikoa minne na kwamba amelipwa shilingi milioni 50 kwa show zote.
Show ya Matumaini 7 July
 kwenye hii show diamond ana zaid ya mil.10

Show ya Kenya 27 July
Kwenye show hii Diamond atashare stage na mastaa wa Nigeria, Ice Prince na Davido na hapa kama alivyosema kuwa katika show za nje ya nchi huwa hachukui chini ya dola 15,000. Kuna uwezekano hapa akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 20.
Kama una calculator basi unaweza ukapiga hesabu mwenyewe ni kiasi gani ameingiza kwa show za June na July. Kumbuka pia kuwa show zote hata za July tayari ameshasaini mkataba na ameshalipwa chake tayari. Kitu kama milioni 140 na usheee!!
Pia kumbuka ni balozi wa Cocacola na hulipwa kila mwezi kwa shughuli zinazohusiana na deal hiyo. Katikati wa mwezi July pia kuna uwezekano akawa na show zingine kibao.
“Siku zote ishi ukikumbuka, Maisha ni Vita, vita ambayo mwisho wake ni siku ya wewe kuingia kaburini, hivyo haupaswi kuchoka wala kukata tamaa.Heshima, Juhudi na Maombi ndio nguzo pekee zitazokusaidia wewe kushinda Vita hii… tambua Mwenyezi Mungu ndiye Muweza na Mpaganga wa yote,” anasema Diamond.