Mwigizaji na mwanamuziki wa mziki wa kizazi kipya baby Madaha ambaye kwa sasa yupo pande za kanda ya ziwa akifanya show maeneo mbalimbali ya mkoa huo anatarajia kuzindua brand yake aliyoipa jina la Amore ambayo itakuwa na viatu, nguo na perfume tarehe 29 mwezi huu kwenye hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na bongomovies kwa simu tokea kahama, baby madaha alisema kuwa huo ni mwanzo tuu na anatarajia kufanya mengi zaidi kwa mwaka huu wa 2013.
“Kwanza nitaanza na nguo, perfume na viatu vinakuja soon, brand kama kawa ni Amore”
“Nimeamua kuingia rasmi kwenye ujasiriamali, pamoja na movie na muziki nataka nifanye na kitu kingine tofauti kidogo, mambo yanabadilika!” Huwezi jua kesho itakuaje alisema baby madaha
“Nakuja na viatu, perfume na nguo za brand ya Amore, kwa sasa vitu hivi vipo kwenye production stage ila tarehe 29 hiyo tukutane pale regency kwa uzinduzi rasmi” aliongeza madaha
SOURCE:Bongo Movies.com