its FAIZA KESSY
Saturday, May 25, 2013
Thursday, May 23, 2013
Wednesday, May 22, 2013
PICHA NA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA VURUGU ZA MTWARA
Taarifa zinaripoti kwamba hali sio
nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya
machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa
hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na
Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali
kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali
kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera
inayosimamia nishati hiyo. Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa
serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam.
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es
salaam. Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu
mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi) Jengo
la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. Lodge/Hotel (Shengena)
inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU)
kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa
moto. Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika. Nyumba kadhaa
za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari
haijathibitishwa rasmi) Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo
yanapata wakati mgumu kupitakwasababu ya mawe na magogo makubwa
yaliyowekwa na Wananchi. Askari kadhaa wamekufa (habari hii
haijathibitishwa rasmi) Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari
kwakuwa wamepita jirani na gari yao. Yadaiwa askari wengi waliokuja si
wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia hovyo.
Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia. Vituo vya Redio vya
Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine
vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa
takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa. Wakati waziri wa Nishati
akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni
"Gesi haitoki hata kwa bomba la peni" Wananchi walalamikia kituo cha
Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala
kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. Hatimaye hivi Punde matangazo
yarejea. Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea
kujadiliwa muda huu Bungeni. Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae
ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.
Tuesday, May 21, 2013
UTATA WA TOUR YA JAY Z TO TZ
Bado wataalam wa mambo wanaendelea
kutofautiana kuhusu ratiba ya Tour ya Jay – z iliyotolewa na Billboard
hivi karibuni katika ratiba hiyo imeandikwa Jay z atatua katika miji 7
ya Africa ikiwemo jiji la Dar es salaam Oktoba 4 mwaka huu pale Diamond
Jubilee. Ratiba hiyo inatia shaka kwa sababu Jay z aliperform tarehe na
mwezi kama huo Dar es salaam mwaka 2006 na katika website ya Jay za
ametoa ratiba ya Tour zake laini ameishia kuandika mwezi Septemba
hajaandika mpaka Oktoba kama walivyoandika Billboard.
SOURCE:Dj Fetty
SOURCE:Dj Fetty
NEW VIDEO:TZ ALL FEMALE STARS-KIDOLE KIMOJA (FISTULA OFFICIAL VIDEO)
Tz All Female Stars
Kidole Kimoja.(FESTULA)
Studio:Surround Sound Studio
Prod:Nash Designer
Dir:Sadiki Hamadi & Peter Mbogo
Redline Production
Kidole Kimoja.(FESTULA)
Studio:Surround Sound Studio
Prod:Nash Designer
Dir:Sadiki Hamadi & Peter Mbogo
Redline Production
SABABU ZA MSANII PROFESA JAY KUCHUKUA KADI YA CHADEMA....HIKI NDO ALICHOKISEMA
Mh Sugu,Profesa Jay na Mh John Mnyika leo Dodoma.
Profesa Jay amesema yeye ni
mwanaharakati muda mrefu na amejiunga na amejiunga na CHADEMA rasmi
leo lakini yeye ni mfuasi wa Chama hicho muda mrefu kutokana na
harakati zake za kutaka kuikomboa Tanzania.Profesa Jay alisema kuwa
anapenda Tanzania Bora,na anaamini Chama cha Chadema kina muelekeo
huo wa kuipeleka Tanzania kuwa Bora.Hiyo ndo maana ameamua kuchukua
kadi ya chama hicho na si kwa nia ya kufanya Siasa ila ni kwaajili ya
kuijenga Tanzania na kuendeleza harakati.
Sunday, May 19, 2013
PHOTOS:Kanye West New Album Art is…Interesting
Subscribe to:
Posts (Atom)