Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Friday, September 6, 2013

Picha + Video :Vurugu za jana Bungeni


Hapa Mhe.Sugu akitolewa njeWakivutana vutana
Mhe.Sugu Akijizuia kutoka huku akingangania kipaza sauti.
Video yenyewe


Wednesday, August 7, 2013

VIDEO:TUKIO ZIMA LA MOTO UWANJA WA NDEGE JOMO KENYATTA LEO ASUBUHI.


Hii ni video ya tukio zima la mlipuko wa moto uliotokea leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta

Wednesday, July 24, 2013

Inspired By Technology:Sasa waweza kupima Malaria kwa kutumia Hii Application|Soma Zaidi Hapa.


mini-IMAGINE2-e1374124657569
Sanyansi na teknolojia ndio vitu vinavyo run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana na ugunduzi ambao Microsoft wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola za Kimarekani elfu kumi na mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo, hivi sasa inawezekana kupima malaria bila hata kutoa damu lakini hapohapo doctor wako akatumiwa taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya  Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu kwa sasa inafanya kazi  na windows phone lakini ili uweze kupima malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.
safe_image 
Credits:Millard Ayo

#SIMCARDTAX:RAIS KIKWETE|SOMA ALICHOKISEMA

B
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam  Julai 23, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.



Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.



Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.



Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.



“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,”Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.



Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.



23 Julai, 2013

Saturday, July 20, 2013

PICHA:MAPOKEZI YA WANAJESHI WALIOUAWA HUKO DARFUR SUDAN.

 
Miili ya wanajeshi saba mashujaa wa Tanzania waliofariki wakiwa kazini wakitekeleza ulinzi wa amani wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini Sudan, imewasili leo kwa ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Kaimu Mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili hiyo imewasili leo Jumamosi majira ya saa 9.45 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.

Miili iliyowasili ni ya Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.

Shughuli za kuagwa miili ya wanajeshi hao zitafanyika katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa vilivyoko Upanga jijini Dar es salaam.

Kuwapoteza wanajeshi hawa ni la kwanza na kubwa kwa nchi ya Tanzania tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007. Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walifariki dunia mwezi uliopita baada ya chombo chao cha kusafiria kusombwa na maji ya mto uliokuwa umefurika huko nchini Sudan. 


Baadhi ya picha za mapokezi yao.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Friday, July 19, 2013

NAMBA ZA SIMU ZA MAWAZIRI ILI KUWATUMIA MAONI KUHUSU KODI YA SIMU


Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644. Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa. 



Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013

Thursday, July 18, 2013

RAIS KIKWETE AMTAKA RAIS WA SUDAN AWASAKE WATU WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA HARAKA IWEZEKANAVYO


Rais Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan, Omar Bashir, kuhusu kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur.

Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Rais  Kikwete alimtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu, na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

Rais Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alimueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini waliohusika ni wahalifu, kusisitiza kuwa lazima watasakwa hadi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Alimpa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha, ambapo wanajeshi wa Tanzania walienda nchini Sudan kulinda amani na usalama wa wananchi wa Sudan.

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha, ambao umewatokea Watanzania hao wakati wakitekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichokiri kuhusika na shambulio hilo, ingawa kumekuwa na hali ya kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na vya waasi katika jimbo la Darfur.

Mapigano baina ya vikundi vya kikabila na koo mbalimbali, yamesababisha mapigano na uvunjifu mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa.

Mara nyingi mapigano na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.

Mwishoni mwa mwaka jana wanajeshi wanne kutoka Nigeria, waliuawa karibu na El Geneina, Magharibi mwa Darfur, ambapo pia inaelezwa na AU kuwa wanajeshi wapatao 50, wameuawa tangu kikosi hicho cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID), kianze operesheni yake mwishoni mwa 2007.
 

Taarifa za UN pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania Jumamosi iliyopita, wanajeshi sita wanaolinda amani waliuawa tangu Oktoba mwaka huu, ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao.
Hata hivyo, kiini cha mgogoro huo inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

Miili ya maaskari hao saba wa Tanzania, inatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa, Julai 19 kwa ajili ya maziko.
Credit:Gumzo La Jiji

HAPPY 95th BIRTHDAY NELSON MANDELA (MADIBA)

 




Afrika Kusini leo wanasherehekea miaka 95 ya kuzaliwa kwa Mzee Nelson Mandela huku rais huyo wa zamani bado yuko mahututi hospitalini.
Ilikuwa ikitabiriwa kwamba shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwamba angeruhusiwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini bado yuko hospitali kutokana na kurejea maambukizi kwenye mapafu.


Kituo cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela na makundi mengine yamewataka watu kujitolea kwa dakika 67 kwa kazi za hisani kukumbukia miaka 67 ambayo Mandela aliitumikia jamii yake.

Umoja wa Mataifa pia umetambua mapambano ya Mandela dhidi ya ubaguzi wa rangi na kusema siku yake ya kuzaliwa ni fursa ya kuenzi urithi wake, na shughuli mbalimbali zimeandaliwa duniani kote.

Siku ya kuzaliwa Mandela, Julai 18, ilitangazwa rasmi kuwa Siku ya Kimataifa ya Mandela na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2009 kama kutambua mchango wake kwa utamaduni wa amani na uhuru.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alisema Siku ya kuzaliwa Mandela mwaka huu imekuja katika wakati wa 'kuakisi kwa kina maisha yake na kazi ya Madiba, huku kiongozi huyo wa aina yake akiwa bado yuko hospitalini'
Aliongeza: "Nelson Mandela alijitolea miaka 67 ya maisha yake kupigania haki za binadamu na haki kwa wote."


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ataadhimisha siku ya kuzaliwa Mandela kwa kutoa michango ya nyumba kwa familia masikini katika eneo la Pretoria.

Mandela alilazwa hospitali mjini Pretoria Juni 8 kwa matatizo ya maambukizi kwenye mapafu yake.

Mapema wiki hii, Rais mstaafu Thabo Mbeki alibashiri kwamba Mandela anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali mapema na kwenda kupatia nafuu nyumbani.

Marafiki ambao walimtembelea wamesema yuko kwenye mashine ya kusaidia maisha kwa ajili ya kusaidia tu kupumua kwa urahisi.
 

Taarifa rasmi za hivi karibuni kabisa kuhusiana na afya yake zilisema Mandela alikuwa kwenye hali mbaya lakini inayoimarika.

Lakini wote, mke wa Mandela, Graca Machel, na Rais Jacob Zuma wamesema hivi karibuni kwamba Mandela anaendelea vema na matibabu.

Shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi alitumikia miaka 27 gerezani kabla ya kuja kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994

Monday, July 15, 2013

PICHA:WANAJESHI 7 WA TZ WALIOFARIKI DARFUR WAKIAGWA HUKO TAYARI KWA KUSAFIRISHWA

Hundreds of UNAMID Sector South HQ staff members led by Head of Office Mr. Imtiaz Hussain today attended a brief ceremony at the Pakistan Level III Hospital in Nyala to pay their final respects to the seven Tanzanian peacekeepers who were killed near Khor Abeche in an ambush by unidentified gunmen on Saturday 13 July 2013.Their bodies were flown today to Khartoum en route to Tanzania.
Top Sector leadership led by Mr. Hussain (3rd R)
UNAMID JSR Dr. Mohamed Ibn Chambas along with Acting Force Commander Lt. Gen. Wynjones Kisamba and Police Commissioner Ms. Hester Adriana Paneras visited the other 17 injured peacekeepers at the same Hospital yesterday.

The Mission leadership and the UNSG Ban Ki-moon have condemned the act and called for the Government of Sudan to bring the perpetrators of the “heinous” act to justice.Meanwhile, according to press reports, Tanzanian President JakayaKikwete expressed his deep shock following the incident and he sent condolences to the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) and the bereaved families.
Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony

He wished quick recovery for the injured soldiers, saying: “I don’t have a lot of words to express my shock and sadness on the soldiers who died while on a very important mission of United Nations, on keeping peace in an area where thousands of people have been killed…” Mr. Kikwete said in a statement issued by the Directorate of Presidential Communications yesterday, adding; “since the fallen servicemen and women were deployed in Darfur in February this year and since Tanzania  started deploying troops in 2007, they have done a good work and the country is proud of them”. 
A portion of  staff members at the ceremony

The TPDF Spokesperson, Lt. Col. KapambalaMgawe, said during a press conference yesterday that a special delegation has been sent to Khartoum and Darfur to talk with the authorities over the incident. Tanzania has a battalion of about 850 peacekeepers in Darfur located at Khor Abeche and Menawashi, South Darfur State.

Military salute as the 'Last Post'  rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers
Prayers from a chaplain
Prayers from another  chaplain
Maj. Elinami Moshi reads brief CVs of the deceased to the top brass
A section of the top brass
Last Post
Start of the last journey home
Credit:Michuzi Blogs & TZ Daily Eye

Sunday, July 14, 2013

MAJINA SABA YA WANAJESHI WA TANZANIA WALIO UAWA HUKO DARFUR SUDANI


Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa  kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.


Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati  wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
 
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

PICHA:Uchaguzi Mdogo ARUSHA