Wednesday, July 24, 2013
NEW VIDEO:Beeman feat wyre - Kizunguzungu|Good Music|All the Way From Arusha
Beeman feat wyre - Kizunguzungu
Cpwaa Breaks|Sasa nyimbo zake zaanza patikana on "iTunes"....Check out hapa
Cpwaa anakwambia…. Ninayo furaha kuwajulisha kwamba sasa kazi zangu zote za muziki zitakuwa zinapatikana kwenye mitandao yote ya kununua nyimbo za wasanii duniani. Tayari nishasambaza Album yangu ya kwanza ” Pwaa The Album” na singles zingine kama “Hmmm”, na “Mambo” kwenye mitandao ifuatayo:
iTunes, Amazon MP3, Spotify, Google Play, Xbox Music, Deezer, Rhapsody, Simfy, MySpace Music, Nokia, Wimp, Sony Music Unlimited,Napster, Verve Life, Media net, Shazam,eMusic, iHeartRadio, Muve Music, and Rdio.
kwa wale mliokosa nafasi ya kujipatia nakala za album yangu ya kwanza, hii ni fursa kwenu kujipatia Album hiyo kupitia mitandao hii kwa bei nafuu sana. Tupeane support ili tukuze muziki wetu.
kwa sasa namalizia kurekodi album yangu ya pili ambayo ipo kwenye mahadhi ya kimataifa zaidi na punde ikikamilika ntaanza kuachia single moja moja kupitia mitandao hii, mitandao ya simu kwa njia ya RBT na pamoja na wa “The Kleek” chini ya mkataba wangu mpya na Universal Music Group.
Asanteni sana na hii hapa ni link ya kupata nyimbo zangu zote kupitia iTunes, https://itunes.apple.com/
Inspired By Technology:Sasa waweza kupima Malaria kwa kutumia Hii Application|Soma Zaidi Hapa.
Sanyansi na teknolojia ndio vitu vinavyo
run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana na ugunduzi ambao Microsoft
wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola za Kimarekani elfu kumi na
mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo, hivi sasa inawezekana kupima
malaria bila hata kutoa damu lakini hapohapo doctor wako akatumiwa
taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka
Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za
kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na
kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama
inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya
malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu
kwa sasa inafanya kazi na windows phone lakini ili uweze kupima
malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.
Credits:Millard Ayo
#SIMCARDTAX:RAIS KIKWETE|SOMA ALICHOKISEMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa
waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya
Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es
salaam Julai 23, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika
na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini
kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya
ya kadi za simu hizo za mikononi.
Rais
kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013
wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu
ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja
kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais
Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara
hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya
kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo
kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa
na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya
Mwaka 2013/2014.
Rais
Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena
kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata
fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge
limezipangia matumizi.
“Nawaombeni
kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja
tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo
tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa
pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,”Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Katika
Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh.
1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya
mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
23 Julai, 2013
PICHA NA VIDEO:PRINCE William& Kate Middleton wakimuonyesha mtoto wao Hadharani.
Hapa Kate Middleton na mtoto wake aliyepewa Jina la George Alexander Louis Siku Mbili baada ya kuzaliwa kwakePrince William akiwa na familia yake saa24 baada ya mtot wao kuzaliwaHali ilivyokuwa njee ya hospitali St.Marry's Hospitalhapa wakiondoka Hospitalini Hapo Video ya tukio zima angalia hapa chini
Ney Lee - Nipe Muda
Staa wa Ngoma ya Umekweenda alichipukia kutoka kwenye Fiesta Super Nyota na kufanya vizuri sasa aachia another Hit Song NIPE MUDA Isikilize hapo chini.
FiDO & Danger Ranger - Tupo Tulipo (Official Music Video) Another HipHop MUsic From Arusha.
Artist:FiDO & Danger Ranger
Song:Tupo Tulipo
Audio:MAJEMBE RECORDS.
Video:Good Pictures Lab (First Music Video Project)
Please leave up your comments.
PICHA:UKIONA HII DRESS CODE UJUE INAWAKILSHA ARUSHA|Unga Ltd
Hapo Kuanzia Juu ni Boshori,DoggyDoggy+Denim Shirts na Chini Trouser Mnyonyo na Converse All Star Oversive Wanasemaga haina Gweraaaa
MUSIC VIDEO:ZaiiD - WHO DAT(Bongo version) Shot in Iringa Ni nzuri good idea.
ZaiiD - WHO DAT(Bongo version)
Subscribe to:
Posts (Atom)