Dongo janja ambae kwa sasa yuko chini ya usimamizi wa Mtanashati
Entertainment na Ostz Juma na musoma, ameshadondoka nchini Africa ya kusini
kwa ajili ya kuanza kazi moja tu ambayo imempeleka huko, ikiwa ni makamuzi
kwa kwenda mbele, na akisisitiza kuwa show yake ya kwanza itafanyika ndani
ya cape town.
janjaro anaonekana kwenye picha kupokelewa vizuri na mashabiki wake na
watanzania waliopo huko, na baada ya kufumbua macho kwa mara ya kwanza na
kuyasafisha kwa majengo mazuri na hali ya hewa tofauti na home, aliamua
kuwapa moyo vijana wenzake kupitia ukurasa wake wa facebook
SOURCE:Dj Fetty
No comments:
Post a Comment