Licha ya kujulikana kwa kufunguka na kuweka wazi mambo mengi ya kimapenzi
katika nyimbo zake, nguli wa r&b Neyo ameweza kuficha siri yake kubwa kwa
miaka mingi.
TMZ wameripoti kuwa Neyo amefunguka kuwa alishawahi kuoa akiwa na miaka
19, lakini ndoa yake haikudumu na ilivunjika kwa mda mchache baadae kwa
kuwa alikuwa akipenda kuingia katika kazi ya muziki lakini mke wake alikua
hataki kabisa na hakuwa akimpa sapoti.
"sasa hivi nipo hapa nilipo, na sijui yeye yuko wapi" alisema kwa utani.
kwa hivi sasa mshindi wa tuzo za Grammy, ameshaendelea na maisha yake ya
kimapenzi
SOURCE:Dj Fetty
No comments:
Post a Comment