MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo ameamuru polisi kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
pamoja na wanafunzi walioshiriki kurusha mawe baada ya kutokea vurugu
zilizotokana na kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Uhasibu
Arusha, Henry Kago (22).
Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu
Arusha, Faraji Kasidi jana alitangaza kufunga chuo hicho kwa muda
usiojulikana kutokana na vurugu zilizotokea chuoni hapo, ikiwemo
ukiukwaji wa nidhamu na urushwaji wa mawe uliofanywa na wanafunzi hao
kwa Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama.
Mulongo alitoa amri hiyo baada ya Lema kudaiwa kuingia chuoni hapo jana asubuhi na kufanya siasa bila kufuata utaratibu.
“Si jambo jema kwa Mbunge kuingia
chuoni na kuhamasisha siasa kwenye jambo hilo la kifo badala ya
kuwatuliza wanafunzi ili tujue kiini cha tatizo hili," alisema mkuu wa
mkoa na kushutumu kwamba jambo hilo linabadilika badala ya msiba
linawekwa chuki za siasa na wanafunzi nao kuingia kwenye mkumbo.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, upo utata
wa kifo cha Kago kutokana na wengine kudai ameuliwa na bodaboda eneo la
Esami na Kanisa la Waadventista Wasabato karibu na chuo huku wengine
wakidai alitoka eneo la Bugaluu.
Alisema polisi inachunguza utata wa kifo hicho cha mwanafunzi huyo aliyekutwa na simu yake ya mkononi.
"Naagiza polisi kumkamata Lema popote
alipo na wanafunzi wengine pamoja na wakili wake,” alisema Mkuu wa Mkoa
bila kutaja jina la wakili.
Baada ya kushawisha wanafunzi hao waandamane au mkuu wa mkoa aje ndani ya nusu saa,Mkuu
huyo wa mkoa alifika chuoni hapo nakutaka kuzungumza nao ndipo wanafunzi hao walipoleta vurugukwa madai amewadharau na vurugu hizo kutulizwa na FFU na Mheshima GODBLESS LEMA kukimbilia pasipo julikana na kutelekeza gari lake,Nakuchukuliwa na BREAKDOWN kama linavyoonekana pichani kupelekwa kituo cha polisi
No comments:
Post a Comment