Taarifa zinaripoti kwamba hali sio
nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya
machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa
hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na
Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali
kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali
kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera
inayosimamia nishati hiyo. Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa
serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam.
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es
salaam. Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu
mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi) Jengo
la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. Lodge/Hotel (Shengena)
inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU)
kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa
moto. Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika. Nyumba kadhaa
za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari
haijathibitishwa rasmi) Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo
yanapata wakati mgumu kupitakwasababu ya mawe na magogo makubwa
yaliyowekwa na Wananchi. Askari kadhaa wamekufa (habari hii
haijathibitishwa rasmi) Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari
kwakuwa wamepita jirani na gari yao. Yadaiwa askari wengi waliokuja si
wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia hovyo.
Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia. Vituo vya Redio vya
Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine
vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa
takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa. Wakati waziri wa Nishati
akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni
"Gesi haitoki hata kwa bomba la peni" Wananchi walalamikia kituo cha
Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala
kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. Hatimaye hivi Punde matangazo
yarejea. Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea
kujadiliwa muda huu Bungeni. Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae
ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.
No comments:
Post a Comment