Showing posts with label TID. Show all posts
Showing posts with label TID. Show all posts

Monday, June 3, 2013

LADY JAYDEE NA T.I.D WASAMEHEANA BAADA YA KUZINGUANA KISA SHOW YA JIDE

Wakati mwingine matatizo hukutanisha watu waliokosana na kuufufua tena urafiki wao. Harakati za maandalizi ya mazishi ya marehemu Albert Mangwea zimewakutanisha marafiki wawili walioingia kwenye tofauti hivi karibuni, Lady Jaydee na TID.
Hivi karibuni TID alitangaza kujitoa kwenye show ya miaka 13 ya Jaydee na kuweka sababu tatu. Kutokana na uamuzi huo wa TID, watu walimchukulia kama msaliti kwa Jide aka Anaconda waliyewahi kufanya hit ya pamoja, Understanding.
Hata hivyo Jaydee amesema alikutana na TID kwenye kamati ya mazishi ya Mangwea na kuweka tofauti zao pembeni.
“I met TID kwenye kikao cha msiba wa Ngwair. I love him, forgive him, he’s ma frnd ana matatizo yake pia but not naniliu,” ametweet Jide.

Friday, May 17, 2013

BREAKING NEWS: TID NAE AJITOA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_1r9Bp-F21yharqdzBQUcNCVnAcK17-PVkuokSeh-bj3lKIfd5UAWA7n_ZCHrGM2WNNWTozrvbc1Ne5fr7xSuBT4czJ64n0bc3sP-S134xxfBPobz_lYnfOorS-bHYRIYpaTWQCkpgCG5/s400/DSC05754.JPG
Show ya miaka 13 katika muziki ya Lady Jaydee inazidi kupata pigo baada ya TID kuwa msanii mwingine latest kujitoa kwenye show hiyo.
401187_10150536949328749_793704636_n
Moja ya sababu anayosema TID ni kuwa ana mkataba mwingine wa show unaolipa zaidi.. Sababu ya pili ni kuwa hataki kuwa katikati ya ugomvi wowote.
Hivi ndivyo alivyoandika TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Three reason why i can’t do lady JIDE SHOW ………….No.1 I have better contract pays me better than.No.2 I really don’t want to be between anybody’s conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari…No.3 nataka kuoa muda wangu ndo huu ……………kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been thru same shit.”
Tayari Linah, Barnaba na Matonya wamejitoa kutumbuiza kwenye show hiyo.