Showing posts with label Lady Jay Dee. Show all posts
Showing posts with label Lady Jay Dee. Show all posts

Monday, July 15, 2013

FAHAMU:DUDE AUVAA uYAHAYA KATIKA VIDEO MPYA YA LADY JAY DEE...



Video ya hitsong ya mwanadada komando Lady Jay Dee imeanza kushutiwa leo jioni, na DUDE ndiye aliyevaa uhalisia kama YAHAYA kwenye video hiyo. KAA TAYARI kuiona video hiyo
Credit:The Official A.B '93

Monday, June 3, 2013

LADY JAYDEE NA T.I.D WASAMEHEANA BAADA YA KUZINGUANA KISA SHOW YA JIDE

Wakati mwingine matatizo hukutanisha watu waliokosana na kuufufua tena urafiki wao. Harakati za maandalizi ya mazishi ya marehemu Albert Mangwea zimewakutanisha marafiki wawili walioingia kwenye tofauti hivi karibuni, Lady Jaydee na TID.
Hivi karibuni TID alitangaza kujitoa kwenye show ya miaka 13 ya Jaydee na kuweka sababu tatu. Kutokana na uamuzi huo wa TID, watu walimchukulia kama msaliti kwa Jide aka Anaconda waliyewahi kufanya hit ya pamoja, Understanding.
Hata hivyo Jaydee amesema alikutana na TID kwenye kamati ya mazishi ya Mangwea na kuweka tofauti zao pembeni.
“I met TID kwenye kikao cha msiba wa Ngwair. I love him, forgive him, he’s ma frnd ana matatizo yake pia but not naniliu,” ametweet Jide.

Wednesday, May 29, 2013

Team Anaconda:LADY JAY DEE AMEAHIRISHA SHOW YAKE RASMI

                          
Lady Jay Dee Kupitia EAST AFRICA RADIO  Leo ametangaza kuahirisha show yake ya miaka 13 Rasmi ambayo ilipangwa kufanyika ijumaa hii tar.31 May.

Friday, May 17, 2013

BREAKING NEWS: TID NAE AJITOA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_1r9Bp-F21yharqdzBQUcNCVnAcK17-PVkuokSeh-bj3lKIfd5UAWA7n_ZCHrGM2WNNWTozrvbc1Ne5fr7xSuBT4czJ64n0bc3sP-S134xxfBPobz_lYnfOorS-bHYRIYpaTWQCkpgCG5/s400/DSC05754.JPG
Show ya miaka 13 katika muziki ya Lady Jaydee inazidi kupata pigo baada ya TID kuwa msanii mwingine latest kujitoa kwenye show hiyo.
401187_10150536949328749_793704636_n
Moja ya sababu anayosema TID ni kuwa ana mkataba mwingine wa show unaolipa zaidi.. Sababu ya pili ni kuwa hataki kuwa katikati ya ugomvi wowote.
Hivi ndivyo alivyoandika TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Three reason why i can’t do lady JIDE SHOW ………….No.1 I have better contract pays me better than.No.2 I really don’t want to be between anybody’s conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari…No.3 nataka kuoa muda wangu ndo huu ……………kama nimekukosea captein na madame kazeni but I have been thru same shit.”
Tayari Linah, Barnaba na Matonya wamejitoa kutumbuiza kwenye show hiyo.




Monday, May 13, 2013

LADY JAYDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO.....TAREHE YA KESI YAKE YAPANGWA



 MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. ...


Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. ...


Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. 


Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo...

Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.

Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo.

Kati ya vielelezo alivyopewa na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets!

Taarifa za mwanadada huyo kufikishwa mahakamani hapo, ziliibuka chinichini kwenye mitandao ya kijamii, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baadaye Lady Jaydee alihoji kuwa pengine yeye ndiye anayestahili ‘kukinukisha’ kwa kuwapeleka mahakamani wasanii walio chini ya Tanzania House of Talent (THT), Estarlina Sanga ‘Linah’ na Elias Barnaba ambao anadai aliwalipa kianzio cha shoo yake ya Mei 31, mwaka huu kisha kumchomolea dakika za mwisho

Saturday, May 11, 2013

LADY JAYDEE Asema Mtunzi Mwingine Wa Wimbo JOTO, HASIRA Aibuka ... Alirekodi Toka Mwaka Jana ...

Few minutes ago, mwanamuziki LADY JAYDEE ametangaza kujitokeza kwa msanii ambae anadai alishafanya single yake ya sasa inayojulikana kama JOTO, HASIRA ... Ikimaanisha ni kama JAYDEE ameurudia wimbo huo ...
According to mwanadada huyo, mtu huyo ni kutoka nchi jirani ya KENYA ... Check alichoandika LADY JAYDEE hapa chini ...

NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA LADY JAYDEE NA CLOUDS FM....RUGE AKIMBILIA MAHAKAMANI


IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa