Sanyansi na teknolojia ndio vitu vinavyo
run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana na ugunduzi ambao Microsoft
wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola za Kimarekani elfu kumi na
mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo, hivi sasa inawezekana kupima
malaria bila hata kutoa damu lakini hapohapo doctor wako akatumiwa
taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka
Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za
kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na
kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama
inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya
malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu
kwa sasa inafanya kazi na windows phone lakini ili uweze kupima
malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.
Credits:Millard Ayo
No comments:
Post a Comment