Showing posts with label Shocking. Show all posts
Showing posts with label Shocking. Show all posts

Wednesday, August 7, 2013

VIDEO:TUKIO ZIMA LA MOTO UWANJA WA NDEGE JOMO KENYATTA LEO ASUBUHI.


Hii ni video ya tukio zima la mlipuko wa moto uliotokea leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta

Wednesday, July 24, 2013

Inspired By Technology:Sasa waweza kupima Malaria kwa kutumia Hii Application|Soma Zaidi Hapa.


mini-IMAGINE2-e1374124657569
Sanyansi na teknolojia ndio vitu vinavyo run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana na ugunduzi ambao Microsoft wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola za Kimarekani elfu kumi na mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo, hivi sasa inawezekana kupima malaria bila hata kutoa damu lakini hapohapo doctor wako akatumiwa taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya  Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu kwa sasa inafanya kazi  na windows phone lakini ili uweze kupima malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.
safe_image 
Credits:Millard Ayo

Saturday, July 13, 2013

HUYU NDIYE BABU ANAYETAKA KUMFUFUA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ILI ASIMAMIE UCHAGUZI MKUU 2015, AZUA GUMZO KUBWA..!!


Mzee (pichani) aliyeibuka hivi karibuni akidai kuwa ana uwezo wa kumfufua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere amezua gumzo.
 Babu huyo aliibuka katika studio za Kyera FM huko mkoani Mbeya akihitaji msaada wa kumfikisha Butihama alipozikwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999 ili amfufue. 


Mzee huyo alikuwa na ufunguo mkononi ambao anadai ndiyo utakaotumika kumfufua Nyerere. Anaeleza kuwa akishamfufua Mwalimu Nyerere ndiye atakayesimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Tuesday, July 2, 2013

PHOTOS:Facebook C.E.O Mark Zuckerberg Akisherehekea Mtaani Baada ya Sheria Ya ndoa ya Jinsia Moja Kupitishwa.


Mmiliki wa mtandao wa kijamii Facebook CEO Mark Zuckerberg amejiunga na wafanyakazi wa kampuni yake waliozidi 700 katika matembezi ya kusherekea maamuzi ya mahakama kuhusu haki za ndoa ya jinsia moja. Matembezi haya yamefanyika mitaa ya San Francisco Jumapili Asubuh.

Sheria hio inayo sherekewa Imeruhusu wanandoa wa jinsia moja kumiliki leseni ya ndoa ndani ya siku 30 baada ya kuoana. 

Friday, June 28, 2013

MTANZANIA MHITIMU WA CHUO MWAKA JANA (SAADAH) AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YENYE THAMANI YA TSH.MIL 170



pretty saadah
Siku ya graduu yake mwaka jana apooo
A BUSINESSWOMAN, Saada Kilongo (26), appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam yesterday

charged with trafficking narcotic drugs worth more than 170m/-.
Before Senior Resident Magistrate Nyigulila Mwasebo, the accused was not allowed to enter any plea to the charge. She was remanded until July 10, this year, when the case will be mentioned.

SOURCE -ZEDDYLICIOUS

Tuesday, June 25, 2013

HAWA NDIO WAVULANA WA FAMILIA MOJA WALIOTOKWA NA MATITI UKUBWANI, WENZAO WAWACHEKA..!

VIJANA watatu wa familia moja ya  Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.
Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni  Yeuri (17 ), Gabriel (11) na  Daniu Ramírez  (12),  hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo.


Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya  Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta  Pedro Antonio Delgado


aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
 Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.”

SOURCE:GUMZO LA JIJI

MAMA ALIA BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WALIOUNGANA HUKO MBEYA...!


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.Akizungumza na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye ni maskini.
Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.

 Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na mikono miwili kila mmoja.
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani watakavyotenganishwa,” alisema.
Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16, walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa nchini India kwa upasuaji.
 “Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo katika hali hii, ndugu zangu walipokuja hospitalini kuniona akiwema mama yangu walinifariji na kunisihi nisiwachukie nizidi kuwapenda.
“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa wakininyima usingizi kwa sababu wamekuwa wakilala kwa nyakati tofauti.
“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa anawapenda kwani amejua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.

 “Maisha yetu ni magumu kwani tunatoka kwenye familia maskini, kazi yetu ni kilimo cha kutumia jembe la mkono hivyo bado kuna mahitaji mengi nashindwa kumudu. Nichukue nafasi hii kuwaomba msaada Watanzania wote walioguswa na tukio hili,” alisema Grace.
Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Lide (3) na hao mapacha ni uzao wake wa pili.
Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii atume mchango wake kupitia namba 0753308525 ambayo ni ya mumewe au aende kumuona Muhimbili.

SOURCE:GUMZO LA JIJI