Showing posts with label CHADEMA. Show all posts
Showing posts with label CHADEMA. Show all posts

Friday, July 19, 2013

FAHAMU:CHADEMA YAJITOA KUWANIA UMEYA WA ARUSHA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeamua kuachana na kuwania umeya wa Jiji na badala yake kimemwomba Meya, Gaudence Lyimo (CCM), atende haki.

Katibu wa Kanda ya Kaskazini wa chama hicho, Amani  Golugwa alisema jana, kwamba Chadema haina uroho wa madaraka kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali inasimamia vipaumbele vya maendeleo.


Hata hivyo, kauli hiyo inapingana na nyingine ya chama hicho ya wiki hii pia, kwamba ushindi katika uchaguzi mdogo wa kata nne, ni chachu katika msimamo wa chama kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, urudiwe.

Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema, Isaya Doita, ndiye aliyenukuliwa wiki hii akisema hayo, akiamini kuwa Meya Lyimo wa CCM, alichaguliwa kimizengwe.

Baada ya Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa hivi karibuni, kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha, huku CCM ikibaki na viti 12 na TLP sita.
 

Pia Chadema ina nafasi ya kuongeza kiti, kwani ina nafasi moja ya viti maalumu iliyokuwa inakaliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka 2011.

Hata hivyo, pamoja na Chadema kuongoza kwa kuwa na viti vingi vya udiwani jijini hapa, haina uwezo wa kuweka Meya, bila kushirikiana na CCM au TLP.

Chadema ikikosa ushirikiano huo, ushirikiano wa CCM na TLP, utabaki kuwa na nguvu ya kuweka Meya na naibu wake madarakani, huku Chadema ikibaki kuwa kambi ya upinzani yenye nguvu katika Baraza la Madiwani.

Golugwa alisema Chadema haina uroho wa madaraka, bali inataka uchaguzi wa Meya wa Jiji urudiwe ingawa haitaki nafasi hiyo kwa kuwa si kipaumbele chake.
 

"Tunaangalia wananchi wanafikiwaje na maendeleo tuna imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria," alisema Golugwa.  
 

"Hatuna shida na Meya wala hatuna uroho wa madaraka tunachopinga ni upatikanaji wa Meya huyo na tunamtaka afanye kazi zake kwa kusimamia misingi ya sheria na si upendeleo, tunahitaji kuona kila mwananchi ananufaika na maendeleo hadi mitaani," aliongeza.

Pia alikaririwa wakati mmoja akisema ushindi huo unaihakikishia Chadema wingi wa wajumbe katika Baraza  la Madiwani, hivyo kuwa na fursa ya kumwondoa Lyimo madarakani.

Sunday, July 14, 2013

FAHAMU: Matokeo ya Uchaguzi katika Kata Nne za Arusha

Uchaguzi uliofanyika leo Jumapili, Julai 14, 2013 wa kuwapata madiwani wa Kata Nne --Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai-- za mkoani Arusha umemalizika.

Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne kama ifuatavyo:

KATA YA THEMI: CHADEMA 678; CCM 326; CUF 313

KATA YA KIMANDOLU: CHADEMA 2,665; CCM 1,169

KATA YA KALOLENI: CHADEMA 1,019; CCM 389; CUF 169

KATA YA ELERAI: CHADEMA 1,715; CCM 1,239; CUF 213

Vyama vingine vilivyoshiriki vilikuwa ni TLP, CCK na Demokrasia Makini

Thursday, July 11, 2013

FAHAMU:Kauli Ya POLISI Tanzania kuhusu CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami

.
.
Ni kauli ya Polisi kutoka Makao Makuu Dar es salaam na imetolewa kutokana na kauli iliyokaririwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe..
.
.
. 
Credit:Millad ayo

Wednesday, June 26, 2013

CHADEMA WAKATAZWA KUVAA KOMBAT BUNGENI...!!

Kombati za CHADEMA mzozo
Siku moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.

Mbowe na wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.

 
 Uamuzi huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.

Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi yanayohitaji majibu.

Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).

Kipengele hicho cha kanuni kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia.

Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo, lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
 kuchukua hatua ya kuwazuia.

“Zile wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.

Licha ya kanuni hiyo kuwa kimya kuhusu kuvaa sare za vyama bungeni, Joel alisema kuwa uamuzi huo ulikuwa ni busara ya spika wa wakati huo, Samuel Sitta, lakini haujaingizwa kwenye kanuni kimaandishi.

Tanzania Daima Jumatano lilitaka kufahamu ni kwanini uamuzi huo ukaanza ghafla juzi baada ya wabunge wa CHADEMA kurejea kutoka jijini Arusha, na Joel bila kufafanua alisema: “Kawaulize walipanga nini wakiwa Arusha? Ndiyo maana tukaamua kuchukua hatua.

“Bora tukaonekana tumewaonea kuliko kuendelea kufumbia macho kanuni. Tuwe wawazi kombati zao zina nakshi kupitiliza kwa mujibu wa kanuni. Kwanini wakina Halima Mdee na Vicent Nyerere tuliwaacha wakaingia? Mbona kombati za Zitto zinatofautiana na wengine?”
Alipotakiwa kufafanua kama kweli walishaonywa wasivae kombati hizo bungeni,

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CHADEMA, John Mnyika alisema Joel hajui kanuni za Bunge ndiyo maana amekuwa anampotosha spika na viongozi wa Bunge kufanya uamuzi wa ajabu.

“Wametuzuia juzi kwa sababu ya maelezo ya akina Pinda na Serikali ya CCM, sio kwa sababu ya ukiukwaji wa kanuni za Bunge. Kumekuwa na utamaduni wa hovyo wa kutafsiri vibaya kanuni za Bunge kwa lengo moja tu, kuwadhibiti CHADEMA,” alisema.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alitolea mfano akisema kuwa walizuiliwa kuingia ukumbini na askari polisi wasiokuwa na mamlaka ya kuwazuia kuingia ndani bali walitakiwa wasubiri amri ya spika kuwatoa ukumbini ndipo wawatoe.

“Hayo yote hawezi Joel kufahamu, anafanyia uzoefu alioupata wakati anafanya kazi Makao Makuu ya CCM wakati wa Bunge la chama kimoja,” alisema Mnyika.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kuwa walishangazwa na uamuzi huo wakati mavazi hayo wamekuwa wakiyavaa miaka yote na kuingia nayo bungeni.

Lissu alisema kuwa hatua hiyo waliichukulia kama mkakati maalumu wa Serikali ya CCM kutaka kuwazima kabisa kuhakikisha hawapati nafasi ya kuingia bungeni ili kujibu tuhuma walizosingiziwa kuhusiana na mlipuko wa bomu jijini Arusha.

“Sisi hali hiyo tulianza kuishtukia tangu asubuhi tulipoingia kwenye eneo la Bunge, kama mligundua kulikuwa na askari wengi sana kila kona kuliko kawaida kana kwamba nchi imepinduliwa. Kinyume na utaratibu wa kanuni askari wa kawaida wameingizwa hadi bungeni,” alisema.

Hata hivyo, pamoja na uamuzi huo, kanuni za Bunge hakuna mahali zinazuia mbunge kuvaa sare ya chama chake isipokuwa kanuni zimeainisha aina za mavazi ya kuvaliwa na wabunge wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa kanuni ya 149 (3)(b) kwa wanaume wanaruhusiwa kuvaa (i) suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia;

(ii) vazi la kimwambao yaani kanzu rasmi na nadhifu, koti, baraghashia na makubadhi au viatu; (iii) suti kamili ya kimagharibi ya rangi kadiri isiyomeremeta; (iv) koti aina ya blazer na tai, pamoja na suruali yoyote ya heshima; au (v) tarbushi na kilemba cha Singasinga, au kilemba chochote kinachovaliwa kwa mujibu wa masharti ya imani au mila.


UCHAGUZI WA ARUSHA WAAHIRISHWA TENA ILI KUIMARISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU..!!


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.
Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa.
Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai.
Kata zinazohusika ni Elerai, Kimandolu, Thani na Kaloleni. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Lubuva alisema walipotangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Juni 30 waliamini kuwa hali ya utulivu na amani ingekuwa imetengemaa.
“Lakini kwa bahati mbaya tumejiridhisha kuwa hali bado inahitaji kuangaliwa kuhakikisha imerejea katika utulivu wake kikamilifu. “Hiyo haimaanishi kuwa ni mbaya, isipokuwa tumeona bado tunahitaji muda wa kama wiki mbili hivi kuona vumbi lililokuwa likitimka limetulia,” Jaji Lubuva alisema.
Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, wapiga kura hawapaswi kutekeleza haki yao ya kupiga kura katika wasiwasi hivyo ni wajibu wa Tume kuhakikisha unaondoka na wapiga kura wanatekeleza haki yao kwa amani.
“Tunataka watu wajihisi huru wakati wa kupiga kura, ndiyo maana tumeahirisha uchaguzi wa kata hizo kwa mara nyingine. Wanapokuwa na amani na uhuru wapiga kura wanaweza kuchagua wanayemtaka kwa utaratibu mzuri, vinginevyo, shughuli yote ya kupiga kura inaweza kuharibika,” alisema Lubuva.
Aidha, alitaka wagombea na vyama kutoendeleza kampeni kwa sababu kuahirishwa kwa uchaguzi hakumaanishi kuwaongeza muda wa kujinadi au kutafuta wapiga kura wa kuwaunga mkono.
“Muda wa kupiga kura haujabadilika. Vituo vya kupigia kura havijabadilika na vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. 
Waliokuwa katika mstari ndio watakaopiga kura na watakaofika vituoni baada ya muda huo kwisha hawataruhusiwa kupiga kura ili kutoa nafasi ya kura kuhesabiwa,” alisema.
Jaji Lubuva alisema matokeo ya uchaguzi huo mdogo yatatangazwa mapema na taratibu za uchaguzi zitazingatiwa ili kutoa haki kwa wapiga kura na wanaopigiwa kura.
Inadaiwa bomu hilo lililokuwa kwenye mfuko wa plastiki, lilirushwa na mtu asiyejulikana. Waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Amir Ally (7), Judith Moshi na Amir Ally.

"TUTAIFUTA CHADEMA ENDAPO ITABAINIKA KUWA WALIRUSHA BOMU LA ARUSHA WENYEWE"....TENDWA.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa,  amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta.
Tendwa  ameyasema   hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp  kuhusu  hatua  zitakazochukuliwa...
Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Source:Gumzo La Jiji

Thursday, June 20, 2013

HIZI NDIO BAADHI YA PICHA ZA MAZISHI YA WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA...!!


Picha za Mazishi ya mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni I Judith William Moshi, aliye fariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013..



Click image for larger version.   Name: 3.jpg  Views: 0  Size: 71.2 KB  ID: 98626

Tuesday, June 18, 2013

PICHA ZAIDI YALIYOJIRI ARUSHA LEO....Soma yaliyojiri HAPA.

 
 Baadhi ya Viongozi Wa CHADEMA waliohudhuria Katika Viwanja vya SOWETO

Polisi Wakilinda eneo hilo kabla ya Vurugu.
 

d

Matairi yalivyochoma Barabarani na jinsi zilivyofungwa.

Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao.

Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.

Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani hapo ni Tundu lissu, Halima Mdee,Mustapha Akonay Pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
 

Monday, June 17, 2013

PICHA:Yaliyojiri Katika Viwanja Vya Soweto Arusha.....Soma Alichosema Mhe.Mbowe Kuhusiana na Bomu.


Mhe. Freeman Mbowe Akiongea na waombolezaji Leo jioni katika viwanja vya Soweto,Aliwahasa watu kuwa muhusika aliyerusha Bomu hilo wanamfahamu na hawakuwa tayari kumtaja leo pale,na kusihii kuwasubiri wanasheria wakubwa wa Chama kwanza pia alisisitiza kumtaja Muhusika aliyehusika na tukio hilo la kurusha bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika majimbo 5 arusha na kusababisha vifo vya watu watatu mpaka hii leo na wengine 70 kujeruhiwa vibaya kabla ya wao kuondoka Arusha.
Pia alimalizia kwa kuwaambia watu wote waliohudhuria kutawanyika na kurejea Manyumbani kwao kwa Amani na Kurejea Kesho Saa 3 Asubuhi kwa ajili ya misa ya kuwaaga wote waliopoteza maisha katika milipuko huo Uwanjani Hapo. 

 Wafuasi wa CHADEMA Wakisikilza kwa umakini wakati Mhe. Mbowe akizungumza.

Hizi ni Picha za Baadhi ya Wafuasi wa Chadema waliofika Uwanjani hapo.

Sunday, June 16, 2013

Kauli ya Polisi kuhusu bomu kwenye mkutano wa CHADEMA, Arusha.

Picture

DR. MARY NAGU ANUSURIKA KUCHOMWA MOTO NA WAFUASI WA CHADEMA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu pamoja na Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni (CCM), wamenusurika kuchomwa moto na wafuasi wa Chadema usiku wa kuamkia jana.

Tukio hilo lilitokea usiku wa manane, baada ya wafuasi wa Chadema, wakiongozwa na Mbunge wa chama hicho Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse, kuvamia nyumba waliyokuwa wamefikia Nagu na Soni, katika Kata ya Bashnet, Babati Vijijini, mkoani Manyara.

Wafuasi hao wa Chadema wanawatuhumu Dk. Nagu na Soni kukutana katika nyumba hiyo kwa nia ya kupanga mipango ya kutoa rushwa ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata hiyo, unaotarajiwa kufanyika leo, ikiwa ni pamoja na maeneo mbalimbali nchini.

Chanzo cha MTANZANIA Jumapili kilichokuwa eneo la tukio kililidokeza gazeti hili kuwa Dk. Nagu na Soni

walikwenda kijijini hapo usiku, wakiwa na magari mawili, kila mmoja na lake na kufika nyumbani kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Petro Baha, kwa kile kilichodaiwa kuwa ulikuwa ni mpango wa kupita na kugawa fedha kwa wananchi usiku huo, ambapo pia inadaiwa ndani ya nyumba hiyo alikuwepo mgombea udiwani wa Kata hiyo, Nicodemus Gwandu (CCM).

Kitendo cha Nagu pamoja na Soni kuonekana katika nyumba hiyo kiliwashitua wafuasi wa Chadema, ambao baada ya muda mfupi walivamia nyumba hiyo wakiwa na Mbunge wao, Natse, madiwani na msafara wa pikipiki na kutishia kuichoma moto.

Mtoa habari wetu huyo alisema kuwa, wafuasi hao wa Chadema waliweka kambi katika nyumba hiyo kuhakikisha Nagu na Soni hawatoki kwenda kwa wananchi usiku huo.

Chanzo chetu kilisema kitendo cha kuzingirwa huku wakitishia nyumba kuchomwa moto kiliwashitua viongozi hao wa CCM na kuamua kupiga simu polisi, ambao walifika wakiwa sita muda mfupi baadaye kwa ajili ya kuimarisha ulinzi hadi walipotoka jana asubuhi.

Inaelezwa kuwa mgombea wa udiwani wa CCM, Nicodemus, ambaye naye alikuwemo ndani ya nyumba hiyo pamoja na akina Nagu, yeye alifanikiwa kutoroka mapema kwa kuruka ukuta na kukimbia.

Alipotafutwa Dk Nagu ili kupata ukweli kuhusu taarifa hizo, simu yake ya kiganjani iliita bila mafanikio na hata alipotumiwa ujumbe mfupi nao hakujibu.

Kwa upande Soni, alikiri kuzingirwa na wafuasi hao wa Chadema, lakini alikanusha madai ya mkakati wa kutoa rushwa.

“Ni wanachama wa Chadema wakiongozwa na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Natse na madiwani karibia wa kata sita pamoja na msururu wa pikipiki, sisi tulikuja kulala, mimi siku zote huwa nalala kijijini, sasa walikuja wakaanza kupiga yowe, ndipo wananchi wakatoka. Tulikuwa wanne na magari mawili,” alisema Soni.

Akielezea sababu za kwenda kulala katika nyumba hiyo, Soni alisema walifikia hatua hiyo baada ya kuwapo kwa mpango wa Chadema kufanya fujo.

Alisema dalili hizo zilianza kuonekana mapema baada ya Dk. Nagu kuwekewa mawe kwenye daraja la Kambesh, kitendo ambacho kilimfanya ashindwe kuondoka na kwenda kulala alipoandaliwa Soni.

Akifafanua tuhuma kuwa walikwenda kwa ajili ya kutoa rushwa, Soni alisema kama wafuasi hao wana uhakika wathibitishe madai yao.

“Waje wathibitishe rushwa gani ya kuwapatia watu wanne, maana ndio waliokuwemo katika nyumba hiyo, hata mgombea wanayedai alikuwepo alikuja hapo mara baada ya kusikia yowe, wananchi wamesaidia kuwatawanya,” alisema Soni.

Mbunge wa Chadema, Natse alikiri kuwepo katika eneo hilo, baada ya kupatiwa taarifa kwa njia ya simu na wananchi ambao walimweleza juu ya kuwako kwa mpango wa kutoa rushwa uliokuwa ukiandaliwa na Nagu pamoja na Soni.

“Kilichotokea saa 7 usiku tulipigiwa simu na wananchi kuwa Waziri Nagu na Soni walikuwa eneo la Bashnet, ambalo ndiyo ngome yao ya rushwa na walikwenda kugawa huko, lakini walipoonekana tu yowe lilipigwa na watu walikusanyika wakitoka na silaha, ikiwemo mapanga na mikuki,” alisema.

Natse alisema kuwa baada ya taarifa hizo walikwenda eneo la tukio ili kuepusha madhara zaidi, kutokana na wananchi hao kudhamiria kuchoma moto nyumba walimokuwamo vigogo hao wa CCM.

“Tulipofika tuliwatuliza wananchi, lakini waligoma kuondoka, lakini wao (kina Nagu) walikuwa wameshapiga simu polisi. Askari walipofika eneo la tukio tuliwataka wawatoe nje wahusika, lakini walitusihi tukubali wawalinde mpaka asubuhi asitoke mtu, suala ambalo wananchi waliliafiki, huku wao wenyewe wakiendelea kuwepo eneo la tukio kuhakikisha kuwa hawatoki kwenda kugawa rushwa mpaka majira ya saa 11 nilipoondoka hapo,” alisema Natse.

Uchaguzi huo unaofanyika leo katika kata ya Bashnet, unawashirikisha wagombea watatu ambao ni Nicodemus Gwandu wa CCM, Alois Gwandu wa NCCR Mageuzi na Laurent Tara wa CHADEMA, ambaye kabla ya kuhamia chama hicho alikuwa diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya NCCR Mageuz

SOURCE:Mpekuzi

MLIPUKO WA BOMU WASABABISHA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA USOGEZWE MBELE


Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha. 

Akizungumza kwa njia ya simu na Radio TBC FM,kutoka Zanzibari mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi alisema kuwa wameamua kusimamisha uchaguzi huo ili kuwapa nafasi vyombo vya usalama kuchunguza swala hilo.

Alisema kuwa sheria inawapa mamlaka kufanya hivyo pale wanapogundua kuwa hakutakua na uhuru wa mpiga kura kwenda kupiga kura.

Source: Radio TBC FM.