VIJANA watatu wa familia moja ya Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa
baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao
waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.
Vijana hao kutoka katika Jamhuri
ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu Ramírez (12),
hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na
kuondolewa matiti hayo.
Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya
jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe
wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii
yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya Marcelino
Velez Santana nchini humo, Dokta Pedro Antonio Delgado
aliamua
kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
Ramirez,
alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha
kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka,
wote tumefurahi sana.”
No comments:
Post a Comment