Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani
la The New York Times,limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili
yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika
toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi
wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu
kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa
kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi huyo amesema kuwa
Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda
wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo,
Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa
mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema kuwa wakati Rais Obama
akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu
cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa
kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na
mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.
Aliongeza kuwa Julai mwaka jana,
serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la kila wiki la
Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu tukio la
kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu huo na
serikali ya Rais Kikwete.
Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari
yenye makao makuu yake New York nchini Marekani, wiki jana ilimtaka
Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa vyombo vya habari atakapokutana na
Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za
kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na ambayo haikutegemewa wakati bomu la
kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa
CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.
Credit:Zeddylicious
Source: New York times
No comments:
Post a Comment