Showing posts with label Obama to Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Obama to Tanzania. Show all posts
Tuesday, July 2, 2013
GEORGE BUSH NA OBAMA WATAKUTANA ANA KWA ANA KATIKA ARDHI YA TANZANIA LEO

Rais wa Marekani, Barack Obama na mtangulizi wake, George W. Bush, leo wanakutana ana kwa ana kwenye ardhi ya Tanzania watakapoweka mashada kwenye Ubalozi wa zamani wa Marekani uliolipuliwa mwaka 1998.
Rais Obama ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuongoza Marekani, akipokea wadhifa huo kutoka kwa Rais Bush, ambaye aliiongoza taifa hilo kuanzia mwaka 2000-2008.
Kitendo cha vigogo hao kukutana nchini ni cha
kihistoria na kinadhihirisha jinsi Marekani ilivyoipa kipaumbele Tanzania kwa masuala ya diplomasia.
Viongozi hao wawili, wapo Tanzania wakati Rais Obama akimalizia ziara yake ya Afrika na Bush atakuwa na mkewe, Laura, watahudhuria mkutano wa wake za marais wa Afrika unaodhaminiwa na Taasisi ya Bush Foundation.
Pia, Michelle Obama, atahudhuria mkutano huo kabla ya kuondoka kurejea Marekani.
Balozi mbili za Marekani za Dar es Salaam na Nairobi, Kenya zilishambuliwa kwa wakati mmoja Agosti 7, 1998.
Obama ataweka shada kama sehemu ya kumbukumbu ya tukio hilo na Bush ataungana naye katika shughuli hiyo.
Hata hivyo, viongozi hao hawatahutubia wakati wa shughuli hiyo.
Rais Obama ametoa pongezi kwa sera za Bush Afrika hasa kwa kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Hata hivyo, utawala wa Rais Obama umejikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Kuna kamandi ya Jeshi ya Africom, ambayo ina kazi kubwa ya kukabiliana na ugaidi barani humu.
Operesheni kubwa za Africom zipo nchi za Afrika Kaskazini, Somalia na Afrika ya Kati ambako wanamsaka kiongozi wa Kundi la Waasi la Lord Resistance, Joseph Kony.
Mwananchi
TANZANIA YAUMBULIWA VIBAYA NA GAZETI MAARUFU LA MAREKANI
Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani
la The New York Times,limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili
yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika
toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi
wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu
kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa
kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi huyo amesema kuwa
Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda
wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo,
Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa
mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema kuwa wakati Rais Obama
akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu
cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa
kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na
mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.
Aliongeza kuwa Julai mwaka jana,
serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la kila wiki la
Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu tukio la
kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu huo na
serikali ya Rais Kikwete.
Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari
yenye makao makuu yake New York nchini Marekani, wiki jana ilimtaka
Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa vyombo vya habari atakapokutana na
Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za
kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na ambayo haikutegemewa wakati bomu la
kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa
CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.
Credit:Zeddylicious
Source: New York times
Monday, July 1, 2013
OBAMA AMEKWISHATUA NCHINI TANZANIA

Rais wa 44 wa Marekanai, Barrack Obama, ametua nchini Tanzania kwa mara ya kwanza muda huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete yupo katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumpokea mgeni wake huyo.
MAANDALIZI YA KUMPOKEA OBAMA YAKAMILIKA...HIZI NI TASWIRA ZA IKULU LEO
Taswira mbalimbali zinazoonesha
maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama
atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama
ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda
vizuri, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es
salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.

Jengo la Ikulu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.




makundi ya wananchi wa Dar es salaam walikishangilia wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipopita kuwasalimia.
PICHA NA IKULU.
Sunday, June 30, 2013
OBAMA ATOA SABABU ZILIZOMFANYA ASIENDE KENYA KWA SASA... SABABU KUBWA NI KESI YA UHURU KENYATTA NA MAKAMU WAKE
US President Barack Obama said Saturday the “timing was not right” for him to travel to Kenya, his father’s homeland, during his current Africa tour, but he expected to go there many times in the future.
Obama said the new government of President Uhuru Kenyatta was still finding its feet after an election in March, and that Nairobi was “still working out issues with the international community”.
He was referring to a looming trial for Kenyatta and Vice President William Ruto at the International Criminal Court for their alleged roles in deadly violence that killed more than 1,000 people after 2007 polls.
“The timing was not right for me as president of the United States to be visiting Kenya when those issues need to be worked on,” Obama said.
But the US leader said he had visited Kenya multiple times before he was president and expected to return.
“My personal ties to the people of Kenya, by definition are going to be strong and will stay strong,” he said.
Obama’s Africa tour started in Senegal, and he is currently in South Africa. He will wrap up his week-long journey in Tanzania.
Source: Capital fm
Saturday, June 29, 2013
Friday, June 28, 2013
NDEGE NANE ZA OBAMA ZATUA DAR
Dar es Salaam. Makachero wa Marekani
wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama,
ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na
kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha
helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo
meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi
ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza
ziara yake ya kwanza Senegal na anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa
jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili
ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine
mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa
wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema
kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi
cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili
kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa
kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana
na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma
mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu,
ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo
zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za
kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.
Meli za kivita na ndege ya kijeshi
Katika hatua nyingine, meli mbili za kivita ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zimeegeshwa Kigamboni.
“Jamaa wana meli kali kwa kweli, mimi
nimekuwa askari wa Kikosi cha Maji kwa muda mrefu na kufanya mazoezi na
mataifa kadhaa, lakini sijaona meli kama zile.
“Wamarekani wanatisha sana. Meli zao
zina zana muhimu za kivita. Pia wanafuatilia kila kitu kinachoweza
kuhatarisha usalama wao. Hawaamini mtu kabisa wala kudharau chochote,”
aliongeza mtoa habari mmoja.
Ndege ya kijeshi
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kuna ndege ya Jeshi la Marekani lakini imeegeshwa kwenye karakana ya Kikosi cha Anga cha JWTZ.
Ndege hiyo inadaiwa iko nchini tangu
mwanzoni mwa wiki hii, ingawa kuna taarifa kuwa zipo ndege nyingine
ambazo zimekuwa zikitua na kuruka.
“Ndege nyingi za Wamarekani zinatua
nchini kwa kipindi cha wiki mbili sasa, zaidi zinaleta watu, ambao
nahisi ni wale wanaohusika na usalama na mizigo.
“Kimsingi kuna mambo mengi
yanaendelea hapa uwanja wa ndege. Ila msisahau pia kuna ujio wa marais
kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mkutano wa Smart
Partnership ndiyo maana kuna mengi yanaendelea hapa,” kiliongeza chanzo
chetu.
Matapeli waibuka
Kuna habari pia, kuna kundi la watu
limeibuka jijini Dar es Salaam ambalo linataka kutapeli wakazi wa jiji
kwa kutumia mgongo wa ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama.
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu,
Suleiman Kova aliliambia gazeti hili kuwa wamepelekewa kesi tatu za
majaribio ya watu kupora wengine kwa kutumia mgongo wa Obama.
Ziara ya Rais Obama imesababisha
kuongezeka kwa mahitaji ya usafiri na malazi, hali iliyosababisha
kuibuka kwa matapeli wanaowalenga watu wenye magari yenye hadhi kwa
wageni wa nje.
Pia hali hiyo imechangiwa zaidi
kutokana na ugeni wa viongozi wapatao 11 kutoka mataifa mbalimbali
duniani, wanaohudhuria mkutano wa Smart Partnership unaoanza leo jijini
Dar es Salaam.
Kova alisema kundi hilo limekuwa likiwasiliana na watu wanaomiliki magari ya kifahari ili wakodishe magari yao.
Source:Mwananchi
CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD OBAMA
Chuo Kikuu Huria Tanzania
(OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya
Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye
maendeleo ya kukuza uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo
imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa
OUT, Dk Asha Rose Migiro.
“Tumeangalia vigezo vyote muhimu
ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais
huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais
Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na
Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini,
Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada
saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma
kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka
nchini Uingereza,David Mellor.
Wednesday, June 26, 2013
MAREKANI YATAJA SIFA ZA OBAMA KUJA TANZANIA....!!
Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania, hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.
Ukitaka kumfahamu mtu, tazama aina ya watu wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea Tanzania hasa baada ya kupata fursa ya kutembelewa na marais wawili wa taifa lenye nguvu zaidi duniani.
Mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyekuwapo madarakani, Bill Clinton, Agosti 28 hadi 29, 2000.
Pia, nchi ikapata tena fursa ya kutembelewa na
Rais George Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa tena ya
kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama, ambaye atakuwa
ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria kwa bara hili.
Licha ya kuwapo hali ya kutoridhika na hali halisi
ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania,
hali inaonekana tofauti kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya
nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.
Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya
Conference call kutoka Washington, Makamu wa Ushauri wa Masuala ya
Ulinzi wa Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anakwenda
Tanzania kwa sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani Afrika
Mashariki. Alisema Afrika hususan Tanzania, ni moja ya masoko muhimu
yanayoibukia ulimwenguni na Marekani lazima iongeze harakati zake barani
humo.
ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA .
Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo
zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.
“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa
yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya
Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema maofisa hao wanakuja kwa makundi na hivi karibuni lilifika kundi la kusimamia mawasiliano ambayo yatatumiwa wakati watakapokuwa nchini.
“Pia wamechukua kwa muda karakana ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyoko kwenye eneo la Uwanja wa Ndege. Maofisa wa Usalama wa Marekani wanataka kufanya shughuli ndani mle,” alisema Malaki.
Pia, ndege mbovu zilizokuwa kwenye maeneo ya uwanja huo zimeondolewa. Viongozi wa Precision Air hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema ni utaratibu wa kawaida kwa karakana kuazimwa wakati wanapokuja wageni mashuhuri.
“Nafasi ile mara nyingi hutumiwa na maofisa wa usalama pale wanapokuja wageni mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,” alisema.
Alidokeza pia pamoja na ugeni wa Rais Obama, pia kumekuwa kuna presha ya ugeni wa marais wa nchi mbalimbali duniani wanaokuja kuhudhuria mkutano wa Smart Partnership unaonza keshokutwa.
Pia wana kazi ya kuwapokea wake za marais wa Afrika watakaokutana na mke wa Rais Obama, Michelle na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, George Bush, Laura.
Kazi inayofanyika
Ofisa mmoja wa Uwanja Ndege ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema maofisa hao walifanya ukaguzi wa hali ya juu kwenye sehemu mbalimbali za uwanja huo wakitumia mitambo maalumu ya kung’amua mabomu.
“Hawa jamaa wako juu sana katika mambo ya usalama maana wana kifaa cha kuchunguza mabomu hata yaliyo chini ya ardhi,” alisema na kuongeza kuwa licha ya kukagua uwanja huo, pia walikwenda mbali zaidi na kukagua maeneo ya jirani.
Mitambo mbalimbali ya shughuli za usalama imefungwa kwenye eneo hilo la uwanja na maofisa wa Marekani walionekana wakiwa juu ya paa la moja ya majengo ya uwanja huo wakifunga mitambo katika minara mirefu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano.
Yavuruga ratiba za ndege
Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa
kufanya mabadiliko ya ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili
kutoa nafasi kwa anga hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake.
Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo.
“Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema Manongi.
Kutua Senegal leo
Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani
Afrika leo na alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa
za Afrika Mashariki.
Akiwa nchini humo, ratiba inaonyesha kuwa atakuwa na mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Pia ratiba hiyo inaonyesha kuwa atakutana na majaji kutoka mikoa yote ya nchi hiyo.
Pia atakwenda katika Kisiwa cha Goree ambacho kiko kwenye Bahari ya Atlantic na atatembelea Jumba la Makumbusho katika kisiwa hicho ambacho kilikuwa kituo cha kuhifadhi watumwa waliokuwa wanasafirishwa kutoka Afrika kwenda Marekani.
“Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa kabla ya kupumzika kwa muda mfupi na kuanza safari ya kwenda Afrika Kusini,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani.
Mwananchi:
Subscribe to:
Posts (Atom)









cv


