Nyota wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone ameamua kuweka wazi juu
ya suala la yeye kukubaliana au kutokubaliana na kuwekwa kwenye orodha
ya wasanii nyota matajiri barani Afrika kutokana na utajiri wake
alioupata kupitia muziki wake.
Hayo yamesemwea hivi karibuni
kupitia jarida moja la burudani ambalo limenukuu Chameleone akisema kuwa
hayupo tayari kunyanyaswa na mtu yeyote kutokana na kumiliki utajiri
wake alionao kwani yeye kazi yake kubwa ni kuwapa watoto elimu yenye
ubora kupitia muziki wake na sio kujigamba na kubweteka na kauli za
utajiri.
Chameleone
ambaye pia anatarajia kuzindua albamu yake ya nne aliyoibatiza jina
Badilisha, mwezi ujao jijini Kampala amemalizia kwa kusema kuwa yeye
mali si kitu kwake na utajiri mkubwa anaojivunia ni mashabiki wanaopenda
kazi zake.
No comments:
Post a Comment