Saturday, June 29, 2013

#FAHAMU: Mdake Babu Ambaye Ameishika Game Ya Hip-Hop Marekani (greatest of all the times) Kupitia Hapa

Umri wake ni miaka 50 na anafahamika kama Rick Rubin, Jina lake halisi ni Frederick Jay Rubin ama wengine pia wanamfahamu kama DJ Double R, Ni Producer wa miaka mingi ambaye amebobea katika kupika midundo ya Rock, hip hop, heavy metal, country, pop, punk rock, hard rock, blues, world music na post-industrial.




Vyombo anavyopiga ni electric guitar, piano na amekuwa kwenye game tokea mwaka 1982 na amekuwa moja ya waaanzilishi na pia watayarishaji muziki katika labels maarufu kama Def Jam, American, Columbia, Warner Bros.   

Rick amekwishapiga mzigo na wakali kama Run-D.M.C., Jay-Z, Kanye West Linkin Park, Josh Groban, Danzig, The Cult, Slipknot, Adele na wengine kibao na mzee huyu kwa sasa anatokea kwenye headlines mbalimbali kutokana na kuwa moja ya watayarishaji wenye mchango mkubwa sana kwenye kuisuka albam mpya ya Kanye - Yeezus na pia Jay Z - Magna Carta.

Thats Rick....

No comments:

Post a Comment