KALA JEREMIAH NA OMMMY DIMPOZ WAONGOZA KWA KUJINYAKULIA TUZO TATU TATU KILA MMOJA
Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri zaidi kimuziki kwa msanii toka
rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae maombi yake kwa ‘Dear God’ yamesikika na
amepata majibu kwa njia ya kipekee na wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua
tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013.
Kala Jeremiah ametumia
mkuki mmoja kunasa ‘swala’ wake watatu muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa
nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop.
Nguvu ya wimbo huo hapana shaka ndiyo imemuwezesha pia
kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip
Hop.
Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini,
Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town
waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop.
Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic
ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa
Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Selector.
Msanii mwingine wa bongo fleva aliyeng’ara katika tuzo hizo
ni Ommy Dimpoz ambae pia aliondoka na Tuzo tatu, ambazo ni Video bora ya wimbo
bora ya mwaka, wimbo bora wa Bongo Pop ‘Me and You’ akiwa na Vannessa Mdee
ambao pia uliwapa tuzo ya wimbo bora wa kushirikishwa/kushirikiana.
Wasanii na watayarishaji wa muziki wa
bongo fleva ambao kwa mara ya kwanza wameweza kujishindia tuzo za Kili ni
pamoja na kundi la Jambo Squared toka Arusha (Kundi bora la muziki wa kizazi
kipya), Rama Dee ‘Kinega’ (Wimbo bora wa RnB ‘Kuwa na subira).
Wengine ni Amini (Wimbo bora wa Zouk Rhumba ‘Ni wewe’), Recho
(Msanii bora wa kike Bongo fleva), na Nay wa Mitego (Wimbo bora wa Hip Hop ‘Nasema
Nao’). Mesen Selecter (Mtayarishaji chipukizi wa Mwaka), Ali Nipishe (Msanii
bora anaechipukia).
Tuzo hizo zimeshuhudiwa huku mfalme na malkia wa muziki wa
kibongo wakitangazwa kuwa Lady Jay Dee ‘Anaconda’ (Msanii bora wa Kike) na
Diamond Platinumz (Msanii bora wa kiume).
No comments:
Post a Comment