Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangweha.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama
Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi
wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza
umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za
kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini
Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda
nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake
mzazi Mzee Keneth Mangwea.
No comments:
Post a Comment